Dawa za kusisimua misuli zawaponza Maafisa wa riadha Russia


Kitengo cha Maadili cha Shirikisho la Riadha Duniani (AIU) jana kimeliadhibu Shirikisho la Riadha la Russia (RUSAF) kwa kukiuka sheria za matumizi dawa za kusisimua misuli ikiwemo kuzuia uchunguzi.

Adhabu hiyo inahusiana na mwenendo waliouonesha maafisa waandamizi wa RUSAF wakati wa uchunguzi dhidi ya mwanariadha wa kuruka juu wa Russia Danil Lysenko kwa kutotaja mahali alipo.

Rais wa RUSAF Dmitry Shlyakhtin na mkurugenzi mtendaji Alexander Parkin, mwanariadha na kocha wake wote wamefungiwa kwa muda.

Gazeti la Uingereza Sunday Times lilitoa habari mwezi Septemba likidai maafisa wa RUSAF walighushi nyaraka za kuonesha kwamba Lysenko ambaye ni mshindi wa medali ya fedha mwaka 2017 alikuwa mgonjwa sana hivyo hakuweza kusema mahali alipo baada ya kushindwa kupatikana wakati wa kuchukuliwa vipimo vya matumzi dawa za kusisimua misuli kwaajili ya mashindano.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad