DC Mjema Ashiriki Kumtafuta Aliyezama mto Msimbazi


Mtu mmoja mkazi wa Jiji la Dar es salaam, anahifiwa kupoteza maisha baada ya kuzama katika bonde la mto Msimbazi maeneo ya Jangwani.

Imeelezwa kuwa mtu huyo alikuwa katika shughuli zake za Kuokota chupa za plastic katika mtohuo.

Mkuu wa Wilaya ya ya Ilala, Sophia Mjema ameshirikiana kumtafuta mtu huyo na amewataka wakazi wa Jiji kuwa waangalifu ili wasipatwe na madhara kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Mjema amesema kuwa licha ya kuwa jitihada za kumtafuta mkazi huyo hazijazaa matunda, vikosi vya uokoaji vinaendelea kumtafuta.

Aidha amesema kuwa ” Tusiwe Tusiwe tunasema haya maji Ni kidogo Mimi Ni mzoefu, unaweza ukaingiza mguu, tope likakukamata maji yakiendelea kuja Hina ujanja, kitakachotokea Ni Kama kilichomtokea huyu mwenzetu”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad