Deni la TAIFA Laongezeka Kwa Tsh Trilioni 3 Katika Kipindi Cha Mwaka Mmoja



Serikali imesema hadi kufikia Agosti mwaka huu, Deni la Taifa lilifikia Tsh. Trilioni 52.303 kulinganishwa na Tsh. Trilioni 49.283 katika kipindi cha Agosti, mwaka jana ambapo kiwango hicho ni sawa na ongezeko la Tsh. Trilioni 3 katika kipindi cha mwaka mmoja

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango alibainisha kuwa kati ya deni hilo, Deni la Ndani lilikuwa Tsh. Trilioni 14.075 na Deni la Nje Tsh. Trilioni 38.227 na kusema kuwa ongezeko la deni lilichangiwa na kupokewa kwa mikopo mipya kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo

Tathmini ya uhimilivu wa deni iliyofanyika Desemba 2018, ilionesha Deni la Serikali bado ni himilivu katika muda mfupi, wa kati na mrefu kwa viwango vya kimataifa na Serikali inaendelea kuhakikisha deni linakuwa himilivu kwa kuhakikisha mikopo inayokopwa inaelekezwa kwenye miradi ya maendeleo yenye tija kwa Taifa
-
Kuhusu mwenendo wa viashiria vya uchumi, Dkt. Mpango amesema Uchumi wa Taifa umeendelea kuwa imara ambapo katika kipindi cha muongo mmoja uliopita (2009 – 2018), Pato halisi la Taifa lilikua kwa wastani wa asilimia 6.4 kwa mwaka  

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  2. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  3. UGANDA
    Deni la Taifa (SHs) 44,000,000,000,000.00
    Idadi ya Wananchi (No.) 44,270,000.00
    Kila RAIA anadaiwa (Sh) 993,901.06
    Kwa siku RAIA anadaiwa (Sh) 2,723.02
    Kwa kila saa za kazi RAIA anadaiwa (Sh) 340.38

    KENYA
    Deni la Taifa (SHs) 5,007,000,000,000.00
    Idadi ya Wananchi (No.) 52,570,000.00
    Kila RAIA anadaiwa (Sh) 95,244.44
    Kwa siku RAIA anadaiwa (Sh) 260.94
    Kwa kila saa za kazi RAIA anadaiwa (Sh) 32.62

    TZ
    Deni la Taifa (SHs) 52,303,000,000,000.00
    Idadi ya Wananchi (No.) 58,010,000.00
    Kila RAIA anadaiwa (Sh) 901,620.41
    Kwa siku RAIA anadaiwa (Sh) 2,470.19
    Kwa kila saa za kazi RAIA anadaiwa (Sh) 308.77

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad