Godbless Lema 'atumiwa salamu' na Humphrey Polepole



Katibu wa Itikadi na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole, amemtaka Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, kutafuta kazi nyingine ya kufanya kwa kile alichoeleza chama hicho kimejipanga kuhakikisha kinapata ushindi kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2020.

Ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha ambapo amesema amesikia Mbunge Godbless Lema huenda akaenda kugombea Ubunge mkoani Kilimanjaro,

"Tuliambiwa hapa Arusha Mjini ni ngome ya chama fulani cha upinzani, wakati wote Arusha imekuwa ya CCM, nimwambie asijisumbue atafute kazi nyingine ya kufanya ikifika kwenye Uchaguzi wa 2020"

Ikumbukwe Godbless Lema ndiye Mbunge wa Arusha Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), pia Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hivi juzi kati nilikutana nAE KATIKA PILIKA PILIKA za utafutaji wa leseni ya Gereji za kutengeneza mabasi. Lakini Rastamani pia alikuwa akiulizia Dreds za

    kijamaika kazi kwenda mbele akiwasha Gari baada ya kulikarabati. Godilesi oyeee.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad