Hai: Wagombea 110 wa CCM wapita bila kupingwa Uchaguzi Serikali za Mitaa

Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Halmashauri ya wilaya ya Hai,Juma Massatu amesema wanachama 110 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliojitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi ya Wenyeviti wa Mitaa, vijiji na vitongoji wamepita bila kupingwa.

Idadi hiyo ni Kati ya vitongoji 294 ambavyo wanachama wa vyama mbalimbali walijitokeza kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea nafasi hizo ambapo hawakuweza kuchukua na kurejesha fomu hizo.

Tayari Msimamizi huyo was uchaguzi amewatangaza rasmi wagombea hao kuwa ndio washindi katika vitongoji hivyo.

Wakati huo huo Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA  kimewataka Wagombea wa chama hicho kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao wameenguliwa kwa madai kuwa wamekosea kujaza fomu zao kukata rufaa.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Itifaki na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema.

Mbali na hilo CHADEMA wameeleza kuwa wataitisha vikao vya dharura kujadili hali hiyo ambayo wamedai kuwa imejitokeza katika maeneo mengi nchini.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Daah..!!! Mbowe . imekula kwako.

    Meseji sendi... and delivadi.

    Ole Sabaya Hongerana mMama Magwhira.

    Wataisoma namba.

    Sijui godi less Lemwa vp na homa ya ndege. manake ATCL Iamdatisha na Uchaguzi unampa kuweweseka na plesha juu.

    Aisikia Mrisho G. Baba lao. Anauliiza Tembe za Zenadoli ziko wapi.

    Watatuelewa tuu Magumashi wa 2010/15.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad