Hamis wa BSS arudishwa kwenye mashindano hayo, Master J ashangaa kurudishwa kwake


Baada ya kelele za mashabiki wa BSS juu ya muimbaji Hamis kuondolewa kwenye mashindano hayo, hatimaye muimbaji huyo usiku wa jana amerudishwa na Chief Judge, Madam Ritta.


Madam amesema muimbaji huyo ameingia top 20 baada ya mshiriki mmoja kujiondoa kwenye mashindano kutokana na shughuli zake binafsi.

Master J ambaye ni mmoja kati ya majaji wa mashindano hayo alionesha kutofurahishwa na kitendo hicho.

Naye Hamis baada ya kutajwa kwamba amerudi, alipanda stejini hapo na kuyashukuru mashindano hayo.

Awali Madam Ritta alidai mshiriki huyo alishindwa kuendelea na mashindano hayo baada ya ratiba ya BSS kuingilina na ratiba ya shule ya kijana huyo hali iliyoadhiri maendeleo yake katika mashindano hayo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad