Hatimae Jose Mourinho apata kazi,achukua mikoba ya ukocha kwenye klabu hii kubwa Uingereza
0
November 20, 2019
Aliyekuwa mkufunzi wa zamani wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho amakabidhiwa na kuchukua mikoba ya Muargentina Mauricio Pochettino baada ya mkufunzi huyo wa zamani wa Tottenham kutimuliwa kazi.
Raia huyo wa Argentina aliiongoza Spurs katika fainali ya kombe la klabu bingwa Ulaya msimu uliopita ambapo walipoteza kwa Liverpool.
Mourinho ambaye ni raia wa Ureno amekuwa bila kazi ya ukufunzi tangu alipofutwa kazi na United mnamo Disemba 2018.
Hakuna maafikiano yalioafikiwa kati ya Mourinho na Spurs kufikia sasa.
Kumekuwa na ripoti kuhusu kukosana kwa Pochettino na mwenyekiti wa klabu hiyo Daniel Levy , lakini uamuzi huo ulichukuliwa kutokana na msururu wa matokeo mabaya katika kipindi cha miezi kadhaa , kuanzia Februari iliopita.
Mkufunzi wa Bournemouth Eddie Howe, kocha wa RB Leipzig Julian Nagelsmann na aliyekuwa kocha wa Juventus Masimilliano Allegri wote wamehusishwa na uhamisho wa kujiunga na Spurs.
Hatahivyo Mourinho anajiandaa kuchukua ukufunzi wa klabu hiyo na iwapo mazungumzo kati yake na klabu hiyo yatakamilika vyema , tangazo linaweza kutolewa mapema siku ya Jumatano asubuhi muda wa London.
Baadhi ya maafisa katika klabu hiyo wanaendelea kuwa na matumaini kwamba Mourinho huenda akazinduliwa katika mkutano na vyombo vya habari siku ya Alhamisi iwapo mazungumzo yatakamilika vizuri.
Uchambuzi
Spurs haijawahi kumsajili mkufunzi aliye na mahitaji ya kiwango cha juu zaidi kama Mourinho , na wala haijawahi kutumia fedha nyingi kuwanunua wachezaji kama vile alivyozoea katika klabu za Real Madrid na Man United.
Hivyobasi mashabiki wengi watashangazwa kwamba huenda akajiunga na klabu hiyo huku kocha wa RB Leipzig Julian Nagelsman akionekana kijana zaidi na mwenye uwezo wa kuongoza klabu hiyo.
Lakini Spurs katika miaka ya hivi karibuni wametoka mbali chini ya ukufunzi wa Pochettino .
Wana uwanja mpya uliojengwa kwa thamani ya pauni bilioni moja na uwanja wa mazoezi mbali na kufuzu kushiriki katika ligi ya mabingwa mara nne mfululizo huku uuzaji wa baadhi ya wachezaji ukiwasaidia na kuifanya klabu kuwa klabu iliojipatia faida kubwa duniani.
Kwa sasa wana kikosi chenye talanta.
Mourinho amekuwa nje ya ukufunzi kwa takriban mwaka mmoja sasa na huku akiendelea kuishi mjini London, kazi hiyo inamfaa sana.
Tags