IAAF yapunguza vipengele mbio za mita 200 kwenye Ligi ya Diamond

Ligi ya Diamond inayoandaliwa na shirikisho la riadha duniani (IAAF) haitakuwa tena na vipengele vya mita 200, mita 3,000 kuruka viunzi, kurusha kisahani ama miruko mitatu kwenye mashindano ya mwaka 2020.

 IAAF imesema imefanya utafiti juu ya umaarufu wa vipengele hivyo na kuamua kupunguza urefu wa kutangaza michuano kwa dakika 90.

Hata hivyo IAAF imesema inaelewa masikitiko ya wanariadha baada ya maamuzi ya kuondoa vipengele hivyo katika mashindano ya mwaka 2020.

Shirikisho hilo limesema kwenye taarifa yake kuwa vipengele hivyo vitashirikishwa kwenye mashindano maalumu yaliyochaguliwa yakiwemo ya Oslo, Rome, na Doha lakini vitaondolewa kwenye michezo inayotangzwa kwa dakika 90.

 Mwanariadha wa Kenya anayeshika rikodi ya dunia kwa upande wa wanawake Beatrice Chepkoech amesema ameshtushwa na maamuzi hayo, na kusema huo ndio mwanzo wa kuua ajira za wanariadha wanaoshiriki kwenye michezo hiyo tu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad