Idris Sultan amuomba msamaha Rais Magufuli



Mchekeshaji maarufu Bongo Idris Sultan, amemuomba msamaha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, baada ya kufanya kosa la kuhariri picha ya Rais na kuweka sura yake, siku moja baada ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwa Rais Magufuli.

Idris Sultan ameomba msamaha huo, leo Novemba 14, 2019, wakati akizungumza na waandishi wa habari, Jijini Dar es Salaam, ambapo amesema kuwa hakuwa na nia mbaya ya kufanya hivyo bali lengo lake lilikuwa ni kufikisha ujumbe wa kumtakia heri ya siku yake ya kuzaliwa.

"Siku zote sipendi kufanya mambo ya kawaida, napenda kufanya mambo tofauti na ninavyofikiria kwa kutumia sanaa yangu ya ucheshi, kwahiyo siku hiyo niliamua kubadilisha picha yangu na ya Rais  kwa sababu najua kiti cha Urais ni kikubwa sana, ndipo niliamua kubadilisha nafasi, yeye akae kwangu na mimi nikae kwenye kiti chake" amesema Idris Sultan.

Aidha Idris Sultan ameendelea kusema "Nia yangu ilikuwa njema ila kwenye sanaa kama ukimkosea mtu yeyote sina budi kumuomba radhi, kwahiyo picha yangu ambayo nimeiweka kwa kumtakia heri ya siku ya kuzaliwa, kama itakuwa imemkera naomba nimuombe radhi kama Baba yangu, Rais wangu na naongea hivi katika hali ya ubinadamu kabisa" ameongeza.

 

Ikumbukwe kuwa mara tu baada ya Idris Sultan, kuweka picha hiyo mitandaoni siku ya Oktoba 29, aliamuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda, afike kituo chochote cha Polisi kilichokaribu naye, ambapo alitii agizo hilo.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad