Wananchi waliojiandikisha kupiga kura katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa, wametakiwa kutumia turufu ya kura yao kuchagua viongozi wenye weledi watakaoshiriki kuwaletea maendeleo.
Wito huo umetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tamisemi, Mh. Selemani Jafo wakati wahitimu zaidi wa 4000 wa chuo cha serikali za mitaa hombolo wakitunukiwa cheti cha awali, astashahada na stashahada.
Kwa upande wake mkuu wa chuo cha serikali za mitaa Dk. Mpamila Madale, amesema mbali na kuzalisha wataalamu pia wamekuwa wakishirikiana na mamlaka mbalimbali za serikali za mitaa katika kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo inayohusu wananchi.
Awali rais wa wanafunzi AMANI KISWABI ameiomba serikali kuwapa kipaumbele cha ajira kwa wahitimu hususani wa chuo hicho kutokana na kuwa na uelewa mkubwa wa serikali za mitaa.