Jafo awaonya mameneja wa mikoa


Waziri wa TAMISEMI Mh. Selemani Jafo, amewaonya mameneja wa mikoa wa wakala wa barabara mijini na vijijini (TARURA), kuwalazimisha madereva wa ofisi hiyo kuendesha magari yanayotakiwa kufanyiwa matengenezo baada ya kupitiliza muda.

Akizungumza jijini Dodoma wakati anakabidhi magari 22 yenye thamani ya shilingi bilioni 2.2 kwa wakala wa barabara mijini na vijijini (TARURA).

'Madereva ndio wasimamizi wa magari, hivyo kiongozi hutakiwi kulazimisha gari kutembea wakati muda wa kufanyiwa matengenezo umewadia, kwa kufanya hivyo ni kuhatarisha maisha yao', amesema Jafo.

Kwa upande wake mtendaji mkuu wa (TARURA), Victor Seif, amesema magari hayo yatasaidia baadhi ya maeneo ya halmashauri nchini, kufanya kazi kwa ufanisi kutokana na miongoni mwa watendaji kwenda saiti kwa miguu.

Tayari wakala wa barabara mijini na vijiji (TARURA), umekabidhiwa jumla ya magari 48 baada ya awali Mh. Jafo kukabidhi magari 26.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad