Jafo: Muda wa kuchukua fomu hautaongezwa ” Msifunge ofisi”
0
November 04, 2019
Waziri wa TAMISEMI, Suleimani Jafo amesema kuwa serikali haitaongeza muda wa kuchua fomu, hivyo amewataka wananchi watumie vizuri muda uliobaki vizuri japo anatambua kuwa kunachangamoto ambazo zimejitokeza.
Amesema kwa changamoto ambazo zimejitokeza na zimefika ofisini kwake tayari ameshatoa maelekezo ili kusiwepo na ukwamishaji wa mchakato.
Pia amepiga marufuku kwa watendaji katika eneo lolote nchini kufunga ofisi kabla wagombea wanaotarajiwa kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa hawajarejesha fomu zao, labda kama wagombea hao wataenda kabla ya saa 10 jioni.
Baada ya zoezi hilo la kurudisha fomu kuisha ofisi zitapokea mapingamizi na Novemba 7 rufani zitasikilizwa, Novemba 17 kampeni zitaanza rasmi.
ikumbukwe kuwa mwishoni mwa wiki iliyopita Mbunge wa NCCR Mageuzi, James Mbatia alitoa wito kwa ofisi ya TAMISEMI kuongeza muda wa kuchukua na kurejesha fomu ili kufidia siku ambazo changamoto zilitokea.
Uchaguzi wa Serikali za mitaa unatarajiwa kufanyika siku 20 zijazo, na lkuhusisha wapigakura milioni 19.7 nchi nzima ikiwa ni ongezeko la taktibani watu milioni 8 kulinganisha na walioshiriki mwaka 2014 ambao walikuwa milioni 11.8.
Tags