Aliyekuwa Waziri wa Muungano na Mazingira, January Makamba amewapongeza Watanzania kwa kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kuachana na matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo yalianza kupigwa marufuku rasmi Juni mwaka huu.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter Makamba ameeleza licha ya ugumu uliyokuwepo kugipa marufuku ya mifuko hiyo, anaona jitihada hizo zimeweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.
"Watu wengi hawatambui ni jinsi gani ilikuwa ngumu kuachana na bidhaa ambayo kwa ukweli inarahisisha sana maisha lakini ina madhara. Hongera kwa Watanzania kwa kuamua kwa dhati kabisa. Kitu cha muhimu sasa ni kuendelea kuwa macho, kuunganisha mafanikio na tufanye kuwa tamaduni"
Ikumbukwe Julai mwaka huu January Makamba alitenguliwa kwenye nafasi hiyo ya Uwaziri wa Muungano na Mazingira na nafasi yake kuchukuliwa na George Simbachawene. Makamba alihudumu katika nafasi hiyo toka kuingia madarakani kwa Rais John Magufuli.
Januali, Vp mzee na anko wako nchini Au kule Duniani.?
ReplyDeleteWapotezee..Umesha samehewa. Kuwa MWEMA.
Januali, Vp mzee na anko wako nchini Au kule Duniani.?
ReplyDeleteWapotezee..Umesha samehewa. Kuwa MWEMA.