JPM Aapisha Mabalozi 5, Wizi Wabainika Ubalozi Ethiopia
0
November 23, 2019
RAIS John Magufuli leo Jumamosi, Novemba 23, 2019 amewaapisha mabalozi watano katika hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino, Dodoma.
Mabalozi hao ni:
1. Maj. Gen Anselm Shigongo Bahati kuwa balozi Misri.
2. Mohamed Abdallah Mtonga Abu Dhabi.
3. Jestas Abouk Nyamanga (Ubelgiji).
4. Ali Jabir Mwadini (Saud Arabia).
5. Dkt. Jilly Elibariki Maleko (Burundi).
Akizungumza baada ya uapisho huyo, Waziri wa Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi amesema;
“Naomba nichukue nafasi hii kuwapongeza na kuwapa pole mabalozi walioteuliwa na kuapishwa leo. Mheshimiwa rais tumebaini kuwa katika Ubalozi wa Addis Ababa kuwa kuna ubadhirifu mkubwa ulifanyika katika ubalozi huo, na mpaka sasa muambata fedha yupo mikononi mwa PCCB Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa).
“Pamoja na ubadhirifu huo kufanyika, cha ajabu CAG alikuwa anaupa hati safi Ubalozi wa Addis Abbaba. Sasa pamoja na CAG , Serikali tutakuwa tunafanya ukaguzi wa kushtukiza mara kwa mara.”
Naye Rais Magufuli, katika maneno machache aliyoyatoa baada ya hotuba ya Waziri Kabudi, alisema:
“Najua mengi yameshasemwa, kwa kifupi napenda kuwapongeza mabalozi niliowaapisha leo, mkaiwakilishe nchi yetu vizuri na nawapongeza kwa kuwa ndiyo mabalozi wa kwanza kuapishwa hapa Ikulu ya Dodoma” amesema Rais Magufuli.
Tags