JPM Atoa Maagizo Mazito NIDA “Muwape Nauli na Hela ya Gesti”


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi mbalimbali waliomsubiri njiani akilekea Mako makuu ya Nchi Jijini Dodoma.



Katika ziara hiyo, Rais Magufuli amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa NIDA kufika Mkoani Morogoro leo na ikiwezekana akae Mkoani humo hata siku tatu ili kushughulikia tatizo la Watu wengi kukosa vitambulisho vya Taifa huku Mkoa mzima ukiwa na Ofisi moja pekee ya NIDA.



“Nimemtaka Mkurugenzi Mkuu NIDA afike hapa Morogoro ashughulikie hii changamoto ya vitambulisho na nataka huduma hii iende kila Wilaya, haiwezekani Watu wasafiri kutoka Wilayani kuja Mjini au muwape nauli na hela ya Gesti, na hili litazamwe Nchi nzima Watu wapewe vitambulisho.



“Watu wanataka kusajili laini zao za simu na mambo mengine lakini zoezi la vitambulisho linacheleweshwa na Watu wachache, suala la NIDA linaenda polepole sana, Mkurugenzi Mkuu wa NIDA nitahitaji unipe na tathmini ya zoezi lote Nchi nzima,” amesema Magufuli.





Aidha, Rais Magufuli amesisitiza kuwa katika kipindi chake cha uongozi hatopanga bei ya mkulima kuuza mazao yake.

“Wengine wanalalamikia bei ya mahindi kupanda, nataka wakulima washangilie kama bei ya mahindi imepanda, biashara hii lazima iwe huru, bei ya mahindi itajipanga yenyewe, wakati wa kuwapangia bei wakulima kwenye mazao yao umekwisha,” amesema Rais Magufuli.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad