Jux aeleza alivyotajwa kwenye sakata la Ruby


Mkali wa RnB Juma Jux, amesema hana uhusiano wowote wa kimapenzi na Ruby, japokuwa jina lake limetajwa na mzazi mwenza wa msanii huyo aitwaye Kusah

Akizungumza na  EATV & EA Radio Digital, Jux amesema hakuna chochote kinachoendelea kati yake na Ruby zaidi ya kazi na ameshangaa kuhusishwa kuwa naye kwenye mahusiano.

"Hamna kitu chochote kama hicho, nadhani hivyo vitu Ruby mwenyewe aliongea na alieleza hakuna mazoea yoyote zaidi ya kazi, wala mazoea ya karibu sijajua kwanini imetokea hivyo au sababu gani watu wanasema hivyo, hata mimi nilikuta picha zimeunganishwa kwa pamoja" ameeleza Juma Jux.

Jux ameongeza kuwa, "Mimi nina mpenzi wangu, Ruby nilikuwa najua ana mahusiano yake japo sasa hivi nasikia kuna vitu havipo sawa ila hakuna kitu, natamani hizo sababu alizozisema ni zipi ambazo ameziona kama tuna mahusiano, namuheshimu kama msanii na mtu ambaye nimefanya naye kazi na sikuwa hata na dalili zozote za kuwa naye" ameongeza.

Wiki moja iliyopita Ruby aliweka picha na maelezo katika mtandao wa Instagram, kuhusu kilichotokea kati yake na Baba wa mtoto wake, ambapo amesema mzazi mwenzake huyo amemshtumu kuwa anatoka kimapenzi n
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad