JUX amelibariki Penzi la Vanessa Mdee na Rotimi "Wafunge NDOA Muda wa Vanessa Umeenda"

JUX amelibariki Penzi la Vanessa Mdee na Rotimi, amewataka wafunge ndoa. Kwenye mahojiano na XXL Clouds FM leo JUX amesema anafuraha kwa sababu Vee yupo kwenye mahusiano ambayo anaonekana anafuraha.

Pia ameongeza kwa kusema Umri wa Vanessa umeenda sana na mwakani atakuwa na miaka 32 na haitaji tena mwanaume wa kuja na kuondoka hivyo anahitaji [Vanessa & Rotimi] wafunge ndoa kabisa.

"Yupo kwenye sehemu ambayo anafuraha hicho ndio kitu ambacho tulikuwa tunasubiri sisi. Mwakani atakuwa anatimiza Umri wa miaka 32, ni mkubwa hivyo haitaji mvulana tu wa kumchezea kwa huu muda, anahitaji mwanaume ambaye atakuwa naye kwa muda." Alisema JUX na kuongeza;

"Niwe mkweli, Nataka yeye na [Rotimi] waoane, sitaki tena baada ya miaka miwili mitatu, wamalize tu. Mimi sehemu yangu nimecheza." Alimaliza.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad