Kagere, Chama Wampa Mchecheto Mbelgiji Simba


KOCHA Mkuu wa Simba, Mbelgiji Patrick Aussems amefunguka kuwa kati ya vitu ambavyo vinampa hofu kwa sasa ni juu ya wachezaji wake ambao wameenda timu za taifa kwa kuogopa kuwa wanaweza kupata majeraha ambayo yanaweza kumharibia hesabu zake.



Kocha huyo amefunguka hayo ikiwa ni baada ya wachezaji 11 wa kikosi hicho kutimka katika timu zao za taifa kushiriki mechi zilizo kwenye Kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).



Miongoni mwa wachezaji walioenda katika timu za taifa ni Meddie Kagere (Rwanda), Clatous Chama (Zambia), Sharaf Shiboub (Sudan) pamoja na Miraji Athuman ‘Sheva’, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Gadiel Michael, Erasto Nyoni ambao wapo na Taifa Stars.


Kocha huyo ameliambia Championi Jumamosi kuwa, anawaombea wachezaji wake hao warudi wakiwa wazima bila ya kupata majeraha kwa sababu wakipata majeraha watamharibia katika hesabu zake za Ligi Kuu Bara.

“Kitu cha kwanza ni jambo zuri kwao kuitwa katika timu zao za taifa, kwa sababu kulitumikia taifa lako ni jambo la kujivunia kwani ni wachezaji wengi hawaitwi.



“Lakini naamini wakitoka huko watarudi wakiwa fiti kwa asilimia 100, kwa sababu kuna baadhi yao walivyoenda mara ya mwisho walivyorudi hapa hawakuwa fiti sana.



“Ninachoomba kitokee kwao ni kurudi tu wakiwa wazima kwa sababu ikitokea vinginevyo na hivyo itatuharibia hesabu zetu hapa,” alisema Aussems.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad