Kama unaona ndoa imekuwa na matatizo achana nae - IGP Sirro


Mkuu wa Jeshi la polisi Tanzania, IGP Simon Sirro amewaagiza Askari wote Nchini kuwashughulikia kwa nguvu ya kadri Wanaume watakaobainika kuwafanyia ukatili wa kijinsia Wanawake na Watoto.

IGP Sirro ametoa kauli hiyo wakati akizindua Kituo cha Polisi cha Dawati la Jinsia, Mugumu Wilayani Serengeti

"Umemuoa Mwanamke ni makubaliano sio Mtoto wako mnakorofishana unampiga unamfundisha nini? wewe ni nani kwake? kama unaona ndoa imekuwa na matatizo achana nae tafuta mwingine, unamkata sikio unampiga wewe ni nani upo juu ya Sheria," alihoji.

IGP Sirro aliendelea kwa kusema, "Nimewaambia Askari ukimpata Mtu amempiga Mke wake na wewe mshughulikie kwa nguvu ya kadri".
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad