Kamishna mpya wa Kazi aagizwa kushughulikia vibali hewa wizarani


Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli amemtaka Kamishna mpya wa Kazi, Kanali Francis Mbindi kushughulikia changamoto lukuki zinazoikabili Wizara ya Kazi ikiwamo utolewaji wa vibali hewa.

Rais Magufuli amesema hayo leo Jumatatu Novemba 4, Ikulu jijini Dar es Salaam alipokuwa akiwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua mwishoni mwa wiki.

“Kamishna wa Kazi na wewe kasimamie pale kuna changamoto nyingi, kuna vibali hewa, kuna watu wanaletwa kuja kufanya kazi kwamba ni utaalamu ambao haupo hapa nchini wakija wanakuja kuja kuendesha greda, kuja kuuza chips wanawanyima Watanzania haki zao za kufanya kazi.

“Mheshimiwa Marata alifanya kazi yake vizuri ndiyo maana nimekaa muda mrefu nikiangalia nani wa kumpa, nimecheki huko kote nikaona hapa panafaa mwanajeshi aliye na vigezo vyote kwa sababu umesoma vizuri mpaka masters ukaenda kwenye vyuo vya kijeshi Marekani, umefanya kazi vizuri EAC, una cheo kikubwa tu ni kanali, sasa kawanyooshe pale watakuja wengi,” amesema.

Amesema alifurahi wakati Marata akiwa Kamishna kwani alikuwa anapata malalamiko mengi ambapo kwa sasa anataka malalamiko kama hayo yawe mengi zaidi kwani ukilalamikiwa maana yake utakuwa unafanya kazi.

“Ile ofisi kaisimamie kweli kweli isije ikawa tumekupeleka pale mwanajeshi halafu kazi zikawa za ovyo, utakuwa umewaaibisha wanajeshi pamoja na CDF, kwa hivyo vibali vya ovyo ovyo wako watu wanaghushi wanashirikiana na wizara nyingine, kasimamie,” amesema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad