Kampuni ya UBER hatarini kutofanya kazi zake London
0
November 26, 2019
Mamlaka ya kudhibiti biashara ya teksi katika mji wa London(TfL) imesema kwamba kampuni ya UBER haitapewa kibali kipya cha kuendesha shughuli zake za teksi mjini humo kwa sababu ya kutotimiza viwango vya usalama vinavyohitajika.
Kwa mujibu wa sheria, UBER sasa imesalia na siku 21 kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa TfL. Wakati wa kipindi hicho cha siku 21, UBER itakuwa huru kuendelea na biashara zake hadi pale rufaa yake itakapokataliwa.
TfL imesema kwamba haijaridhishwa na juhudi za UBER kulinda usalama wa abiria wake.
“Usalama una umihumu wa juu kwetu. Licha ya kwamba UBER imepiga hatua, hatua hizo hazijaridhisha kwa kuwa bado abiria wanawekwa kwenye magari ambayo yanaendeshwa na madereva wasiokuwa na vibali au bima,” amesema mkurugenzi wa utoaji wa vibali wa TfL, Helen Chapman alisema.
Meya wa London Sadiq Khan ameunga mkono uamuzi wa TfL akisema “katika muda wa miezi michache zilizopita, safari 140,000 ziligunduliwa kuhusisha madereva walaghai ambao huweka picha za za kupotosha na kuhatarisha usalama wa abiria
Tags