Idadi ya watu nchini Kenya imeongeza hadi kufikia milioni 47.564,296 kwa mujibu wa chapisho la matokeo ya idadi ya watu maarufu sensa iliyotewa hapo jana siku ya Jumatatu ukilinganisha na milioni 38.6 ya mwaka 2010.
sensa
Hii ni sensa ya sita kufanyika tangu kupatikana kwa uhuru nchini humo. kwa mara ya kwanza watu wenye jinsia mbili walihesabiwa kama kundi maalum, watu hawa hawapo kwenye kundi la wanaume au wanawake.
Matokeo hayo yalichapishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu Kenya (KNBC), ilisema kuwa wanawake wapo millioni 24 na wanaume wakiwa 23.5 na zaidi ya watu wenye jinsia mbili 1500.sensa
Baadhi ya maofisa wa sensa, wakiwa wanajiandaa na zoezi la kuhesabu watu lilofanyika mwezi Agosti. Mji wa Nairobi pekee ndio wenye watu wengi zaidi, ukiwa na watu milioni 4.4.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyata anasema kuwa idadi ya watu itasaidia sana katika kuandaa mikakati ya maendeleo.
Kenya ilianza zoezi la kuhesabu watu yaani sensa mwezi agasti. Serikali hutumia shughuli hii ili kujua jinsi ya kupanga na kukadiria matumizi ya raslimali na fedha lakini pia wanasiasa hutumia idadi ya watu na maeneo walioko kutathmini azma zao za kisiasa.
katika kipindi cha sensa ya mwaka huu, raia nchini Kenya walitumia mitandao ya kijamii kuelezea kutoridhishwa kwao na hatua ya kufunga maeneo ya burudani ili kufanikisha mpango wa kitaifa wa kuhesabu watu.
Waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang alizua gumzo nchini humo baada ya kutangaza mabaa na kumbi za burudani kufungwa kwa ajili ya shughuli ya kuhesabu watu maarufu sensa.