Kili Queens, Kenya Leo Patachimbika Dar


KILIMANJARO Queens na Kenya, ‘Harambee Starlets’ zitakutana leo katika mchezo wa fainali ya Mashindano ya Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), huku kila timu ikiingia uwanjani na njaa ya kutaka ubingwa.



Kili Queens na Starlets zinakutana katika hatua hiyo ikiwa, kila timu imeongoza katika kundi lake pasipo kupoteza mchezo wowote, Kili Queens waliongoza Kundi A kwa kuvuna pointi tisa, huku Starlets wakiongoza Kundi B wakiwa na alama tisa pia.




Kili Queens wanahitaji kupata ushindi ili kutwaa kombe hilo kwa mara ya tatu mfululizo, huku Starlets wakihitaji ushindi ili kuzima utawala wa Kili Queens na kutwaa kombe hilo kwa mara ya kwanza.



Kocha wa Kili Queens, Bakari Shime, amesema kuwa: “Hii ni hatua kubwa na muhimu kwenye kila timu kwa sababu ni mchezo wa fainali na kila mtu anahitaji kuwa bingwa, sisi tunataka ushindi ili kuweka rekodi ya kuchukua kwa mara ya tatu, huku Kenya wanataka ushindi ili walitwae kwa mara ya kwanza, hivyo mchezo utakuwa mgumu lakini tutawafunga kama tulivyofanya Rwanda.”



Fainali ya Cecafa itapigwa leo katika Uwanja wa Chamazi Complex, kati ya Kili Queens na Starlets saa 10 jioni, huku mchezo wa kwanza utakuwa ni wa kutafuta mshindi wa tatu, Burundi dhidi ya Uganda, utakaochezwa saa saba mchana.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad