Kiti cha Kocha wa Arsenal Chawaka Moto Apewa Wiki Nne

Mkufunzi wa Arsenal Unai Emery amepewa mwezi mmoja kunusuru kazi yake. (Sun)

Manchester City inatafakari uwezekano wa kuweka dau la kumnunua beki wa RB Leipzig Mfaransa Dayot Upamecano, 21, mwezi Januari. (90 Min)

Barcelona imekataa ofa ya karibu £13m, £17m kutoka kwa klabu ya ligi ya premia ya kumnuua kiungo wa kati wa Croatia Ivan Rakitic ambayo haijafikia thamani ya mchezaji huyo wa zamani wa Sevilla wa miaka, 31. (Sport)

Barcelona imekataa ofa ya klabu ya ligi ya premia ya kumnuua kiungo wa kati wa Croatia Ivan Rakitic(kushoto)

Crystal Palace inatarajiwa kuweka dau la £20m kumnunua mshambuliaji wa Celtic raia wa Ufaransa Odsonne Edouard, 21. (Sun)

Real Madrid na Barcelona huenda zikamwania beki wa Inter Milan kutoka Slovakia Milan Skriniar, 24, ambaye pia analengwa na Manchester United. (Corriere dello Sport)

Manchester United na Arsenal zinamfuatilia kipa wa Hartlepool wa miaka 17, Brad Young. (Sun)

Real Madrid na Barcelona huenda zikamwania beki wa Inter Milan Milan Skriniar
Manchester United inajiandaa kufanya mazungumzo na wawakilishi wa Tahith Chong huku klabu hiyo ikijaribu kudhibiti azma ya Juventus kumsaini kiungo huyo wa miaka 19. (Metro)

Chelsea inamtaka mshambuliaji wa Wigan wa miaka 17 - Muingereza Joe Gelhardt, ambaye pia anafuatiliwa na vilabu vya Manchester United, Manchester City, Liverpool, Tottenham na Everton. (Star)

Mshambuliaji wa Juventus na Ureno Cristiano Ronaldo, 34, anasisitiza kuwa hana tatizo lolote na meneja Maurizio Sarri kufuatia matukio ya hivi karibuni yaliochangia kupumzishwa kwake. (Corriere dello Sport)

Cristiano Ronaldo, 34, anasisitiza kuwa hana tatizo lolote na meneja Maurizio Sarri
Eric Abidal amethibitisha kuwa Barcelona wanamtaka kumsajili mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Lautaro Martinez, 22, kuchukua nafasi ya mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez, 32. (Mundo Deportivo)

Mkurugenzi wa michezo wa Barcelona Abidal amemuunga mkono kocha Ernesto Valverde na kupinga madai kuwa klabu hiyo ya Catalan inamtafuta mshambuliaji mwingine. (Sport)

Mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgii Michy Batshuayi, 26, anataka kusalia katika klabu hiyo na kupigania nafasi yake badala ya kuondoka mwezi Januari. (Sun)
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad