Kocha wa Simba SC Patrick Aussems ajibu tuhuma za kufurushwa kazi


Kocha wa Simba SC Mbelgiji Patrick Aussems amethibitisha ameondoka nchini Tanzania kwa siku mbili kwa sababu binafsi na anataraji kurejea kesho kufanya maandalizi ya mechi yao dhidi ya Ruvu Shooting Jumapili hii Novemba 24 mwaka huu.

Kauli ya kocha huyo kupitia mitandao yake ya kijamii amefutilia mbali uvumi wa yeye kuhama Simba SC kimya kimya.

“Niliondoka kwa siku mbili kwa sababu zangu binafsi, itarudi kesho kuandaa timu kwa ajili ya mechi na Ruvu ili tuweze kupata pointi tatu," ameeleza  Patrick Aussems.

Simba SC mpaka sasa wapo kileleni mwa ligi kuu Tanzania Bara,wakiwa wamecheza mechi 9, wakishinda mechi saba, sare moja, wamepoteza mechi moja na kukusanya pointi 22.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad