Kundi la Islamic State Wathibitisha Kifo Cha Kiongozi wake Na Kumtangaza Kiongozi Mpya

Kundi la wapiganaji la Islamic state limethibitisha kifo cha kiongozi wake Abu Bakr al-Baghdadi na kumtangaza mrithi wake.

Kundi hilo la kijihad limetuma ujumbe wa Telegramu ulioandikwa Abu Ibrahim al-Hashemi al-Qurayshi kuwa ndio kiongozi wao mpya .

Abu Bakr al-Baghdadi, kiongozi wa kundi la Kijihad la Islamic State (IS) na mtu ambaye alikuwa akisakwa sana duniani , alijiua kufuatia uvamizi wa Marekani uliotekelezwa na kikosi maalum cha wanajeshi kaskazini magharibi mwa Syria.

Kiongozi huyo aliyejiita 'Kalifa Ibrahim' alikuwa amewekewa dola milioni 25 kwa mtu yeyote ambaye angefichua maficho yake na alikuwa akisakwa na Marekani na washirika wake tangu kuanzishwa kwa kundi la IS miaka mitano iliopita.


Baghdadi aliapishwa kuwa kiongozi wa kundi hilo mwaka 2014 wakati ambao wanamgambo wa IS walipoweza kuishinda Iraq na Syria na kuanzisha utawala wao mpya wao.

Katika ujumbe wa maneno, IS imethibitisha pia kifo cha msemaji wa IS bwana Abu al-Hasan al-Muhajir - ambaye aliuliwa tofauti na operesheni ya Marekani ya tarehe 27 Oktoba.

Raia huyo wa Saudi anatarajiwa kuwa mrithi mzuri wa Baghdadi .

Msemaji mpya wa IS, Abu Hamza al-Qurashi aliitwa pia kuapa kwa waislamu kuwa msemaji mzuri wa al-Qurayshi.

Wakati huohuo Marekani nayo ilionyesha picha ya kwanza ya jinsi walivyomvamia Baghdadi .

Huku rais wa Marekani Donald Trump aliusifu uhuru huo wa Syria lakini akaongezea, tutaendelea kuwa waangalifu dhidi ya IS


Abu Bakr al-Baghdadi, alikuwa kiongozi mkimbizi wa wapiganaji wa Islamic State (IS) na uongozi wake wa kidini amewekewa $25m (£19m) na serikali ya Marekani kwa mtu yeyote atakayempata.

Ni mzaliwa wa Samarra, nchini Iraq, mwaka 1971, Jina lake kamili ni Ibrahim Awad al-Badri.

Akiwa mfuasi mkuu wa dini ya Kiislamu tangu akiwa mdogo, baadaye alikuwa amefungwa katika kambi moja ya Marekani kwa jina Bucca 2004 kufuatia uvamizi wa Ufaransa na Marekani.

Akiwa katika kambi hiyo aliweka ushirikiano mzuri na wafungwa wengine wakiwemo maafisa wa zamani wa ujasusi nchini Iraq.

Alijifunza mengi kuhusu jinsi anavyoweza kufanya operesheni zake kutoka kwa maafisa wa kijasusi wa aliyekuwa rais wa Iraq ,Sadaam Hussein.

Usalama wake ulikuwa ni wa hali ya juu ,kutokana na kiwango cha juu cha wasiwasi alionao.


Alikiri kuhusu kushindwa kwa kundi lake na kusema kwamba IS ilikuwa ikipigana vita vya kupunguza nguvu za adui, akiwataka wafuasi wake kutekeleza mashambulio yatakayowafurusha wapinzani wao, kupitia wanadamu, kijeshi, kiuchumi, na raslimali za kimkakati.

Haikubainika ni lini au wapi kanda hiyo ya video ilirekodiwa, lakini Baghdadi alionekana kuwa buheri wa afya.

Alionekana akiwa ameketi na takriban watu watatu ambao nyuso zao zilikua zimefichwa na kupitia faili za wanachama wa IS katika matawi kadhaa kote duniani.

Pia aliwataka wafuasi kuwaaachilia huru maelfu ya washukiwa wa IS na makumi ya maelfu ya wanawake na watoto wanaohusishwa na IS ambao walikuwa wakizuiliwa katika jela za SDF na kambi za Syria kufuatia kukombolewa kwa Baghuz.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad