Kunguni waibukia jengo la wasafiri Kituo Kikuu cha Mabasi

Jengo la wasafiri Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo Mikoani katika Halmashauri ya Mji wa Kahama mkoani Shinyanga limeanza kufanyiwa ukarabati baada ya kubainika kuwa na wadudu aina ya Kunguni.

Akizungumza na Mwandishi wa Muungwana Blog Mwenyekiti wa kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani Salum Said amesema jengo la wasafiri lilikuwa limechakaa hadi kusababisha wadudu aina ya Kunguni kuvamia hivyo kusababisha wasafiri kupata wakati mgumu wa kupumzika wakati wakisubiri muda wa safari kuanza.

Said amesema Mbunge wa jimbo la Kahama mjini Jumanne Kishimba alitembelea kituo hicho na kuzungumza na viongozi ili kupokea changamoto zilizopo hapo ambapo walimwambia jengo hilo limechakaa na kuahidi kulikarabati mara.

Amesema nyumba za kulala wageni zilizopo karibu na kituo hicho cha mabasi zina gharama kubwa ambazo sio rafiki kwa wasafiri hivyo jengo hilo limekuwa likitumika hivyo kituo hicho cha mabasi ni kikubwa ambacho hupaki mabasi zaidi ya 60 kwa siku.

Kwa upande wake katibu wa mbunge jimbo la Kahama mjini Abdul Mpei amesema mbunge ameamua kukarabati jengo hilo kupitia mfuko wa jimbo ambayo kwa ujumla ukarabati huo utagharimu kiasi cha shilingi 300,000Tshs.

Amesema mbunge alifika na kujionea hali ya kituo cha mabasi pamoja na kupokea changamoto ambapo pia aliahidi kushughulikia suala la taa za kituo hicho kwani zimekuwa haziwaki kwa muda mrefu.

 Aidha mbunge wa jimbo la Kahama mjini Jumanne Kishimba jana ameanza ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kufanya mikutano ya hadhara ya wananchi ili kupokea changamoto ndani ya jimbo lake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad