Kwa shilingi 3000 na 5000 utashuhudia Taifa Stars Vs Equatorial Guinea
0
November 07, 2019
Shirikisho la soka nchini TFF limethibitisha kuendelea vyema na mchakato wa maandalizi ya mchezo wa Kundi L wa kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2021) dhidi ya Equatorial Guinea utakaopigwa Ijumaa ya Novemba 15 kuanzia Saa 1:00 usiku Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Stars itaanzia nyumbani kampeni hizo za kuwania kufuzu fainali za Afrika (AFCON 2021), kisha itasafiri kuelekea Libya kucheza mchezo wa pili utakaopigwa Jumanne ya Novemba 19.
Katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini TFF Wilfred Kidao amesema mipango ya maandalizi inakwenda vizuri, huku akiwataka watanzania kuendeleza uzalendo wa kuishabikia timu yao, kwa kufika uwanjani siku hiyo bila kukosa.
Kidao ametangaza viingilio vya mchezo huo kuwa Shilingi 3,000 kwa mashabiki watakaokaa kwenye viti vya rangi ya kijani na Shilingi 5,000 kwa mashabiki watakaokaa viti vya rangi ya bluu na machungwa.
“Kuelekea mchezo dhidi ya Equatorial Guinea, TFF imeweka viingilio vya chini ili kutoa nafasi kwa mashabiki wengi kujitokeza kushangilia.
Manara ataja ‘point’ wanazotaka kwenye Ligi kuu
“Masuala ya ufundi yanabakia kwa benchi la ufundi. Mchezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania anapokuwa amevaa jezi ya Taifa Stars ni wajibu wetu kumshangilia,” alisema Kidao.
Tags