Kwanini Baadhi ya Binadamu Huzaliwa na Mkia?
0
November 10, 2019
Kila binadamu aliumbwa akiwa na mkia mdogo ambao hufyozwa na kutoweka tangu siku za mwanzo za uhai wake tumboni kwa mama.
Mkia huo ni miongoni mwa viongo ambavyo vipo ndani ya mwili wa binadamu lakini havina kazi yeyote.
Binadamu akiwa katika hatua ya kijusi, huwa na mkia ambao sio wa kudumu na hutengenezwa kati ya wiki ya 5 au ya 6 ya ujauzito na huwa na pingili kati ya 10 hadi 12 za uti wa mgongo.
Jinsi ya kutumia kabichi kama dawa
Japo kuna wanaozaliwa wakiwa na mkia lakini Katika hali ya kawaida binadamu hatakiwi kuzaliwa akiwa na mkia kwani hufyonzwa au kupotea wakati wa mabadiliko ya ukuaji ndani ya tumbo ambapo hutengeneza mfupa (Coccyx), unaopotea ndani ya wiki 8 za kwanza za ujauzito.
Hadi sasa wataalamu wamegundua kuwa sababu kuu ambazo hupelekea mtu kuzaliwa na mkia ni, Upungufu wa Folic acid kwa mama mjamzito, mabadiliko yasiyo ya kawaida ya taarifa muhimu za mwili pamoja na kushindwa kwa chembechembe nyeupe za damu katika kufyonza mkia wote kwenye wiki ya 8 ya ujauzito.
Kwamujibu wa tafiti zilizofanywa, imebainika kuwa watoto wa kiume ndiyo wana nafasi kubwa zaidi ya kupatwa na tatizo hili ikilinganishwa na watoto wa kike.
Chukua haya unapomtembelea mama aliyejifungua, ”Using’ang’anie kubeba mtoto”
Baada ya kuzaliwa mtoto, huonekana mfupa uliochomoza sehemu ya chini kabisa karibu na kiuno (kwenye makalio), mara nyingi huwa hakuna mifupa ndani yake, isipikuwa mishipa ya fahamu na damu inayozunguka ndani yake.
Matibabu ya tatito hili huzingatia madhara yanayotokana na uwepo wa mkia huo. ambapo mtoto anaweza kufanyiwa upasuaji wa kuondoa kulingana na vipimo vitakavyo onesha
Tags