Lema amtaka Polepole agombee naye Arusha 2020
6
November 19, 2019
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, amesema hana mpango wowote wa kugombea jimbo lolote mkoani Kilimanjaro, bali atagombea tena jimbo la Arusha Mjini, na kudai atashinda kwa kishindo..
Mbunge Lema ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na EATV na EA Radio Digital, kuhusiana na kauli iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole, kuwa Mbunge huyo huenda akahamia jimbo jingine kwenye Uchaguzi wa 2020.
Lema amesema kuwa "Kwanza Polepole inabidi afahamu Ubunge kwangu si ajira, naweza kufanya kazi hata nikiwa mtumishi wa Mungu, au Mwalimu wa Sunday School, ila niweke wazi siwezi kwenda kugombea Kilimanjaro, nitagombea palepale Arusha Mjini."
"Tena niwaambie tu nitagombea palepale Arusha Mjini, na niwaambie CCM wamuweke mgombea yeyote yule hata akiwemo yeye mwenyewe Polepole nitamshinda tu." ameongeza Lema.
Novemba 17, 2019 akiwa mkoani Arusha Katibu wa Itikadi na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi Humphrey Polepole, alimtaka Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, kutafuta kazi nyingine ya kufanya kwa kile alichoeleza chama hicho kimejipanga kuhakikisha kinapata ushindi kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2020.
Tags
Nimefurahi kweli, kwa Godilesi kuelewa kuwa Ubunge si Ajira, sielewi kama chamani huo ndio Uelewa wa Wote, na kama siyo basi aanzishe awareness spread Campaign Hasa chamani kwa kuna wsiotaka kuelewa na wanaamini kuwa Ubunge ni Ajira wakiwemo Watoro huko ughaibuni.
ReplyDeleteSasa Rastamani amekossa Vigezo na Sera
ufundi wa Geleji ni Saizi yake.
Polepole anayo Ajira stahiki na anaitendea haki.
Chalenji ulio itoa,huku ukijua fika
kwamba hato ingilia anga hizo.
Haina tafsiri nyingine zaidi ya kujitafutia teke la mitandaoni. Pole Godilesi tena Pole sana. Wana Arusha wamesha Kurusha, Anza kutafuta Ajira.
Swadakta Mdau. Hawa wanachukulia uwakilisshi ni kama AJIRA wanatia ndani Posho.Wenginne Magummashihata Jimboni hawafiki baada ya kupewa ULAJI.
DeleteNimefurahi kweli, kwa Godilesi kuelewa kuwa Ubunge si Ajira, sielewi kama chamani huo ndio Uelewa wa Wote, na kama siyo basi aanzishe awareness spread Campaign Hasa chamani kwa kuna wsiotaka kuelewa na wanaamini kuwa Ubunge ni Ajira wakiwemo Watoro huko ughaibuni.
ReplyDeleteSasa Rastamani amekossa Vigezo na Sera
ufundi wa Geleji ni Saizi yake.
Polepole anayo Ajira stahiki na anaitendea haki.
Chalenji ulio itoa,huku ukijua fika
kwamba hato ingilia anga hizo.
Haina tafsiri nyingine zaidi ya kujitafutia teke la mitandaoni. Pole Godilesi tena Pole sana. Wana Arusha wamesha Kurusha, Anza kutafuta Ajira.
Mdau, huyu kweli ameshikwa naHoma ya uchaguzi.
DeleteAmesha anza kuweweseka hata madam Hero amesema. Anadandia Mada bila Sera. Mara ATCL Mara Demoklasia mara... Simwelewagi.
Mie nilisikia amekwendda Vujo halafu pia kapeleka watu Kiteto kote wamemtolea nje.
ReplyDeleteUshauri wangu kwa huyu dogo.
Jaribu kumuona kamanda Siro akupeleke mafunzoni ili ukifikia ukoplo tuweze kuwasaka washikaji malasta na mateja
Godi changamkia hiyo ajila endelevu.
Hii imemchanganya na kufanya azidi Kuchanganyikiwa Baada ya Kalista Lazaro kusepea huku kwa
DeleteWachapa Kazi na kuondoka toka kwa Magoi goi.