Mbunge wa Arusha mjini (Chadema), Godbless Lema, amemjia juu waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo kwa kumtaka aache kuongea kama kijana anaye balehe kwani chanzo cha amani duniani ni dhuluma katika uchaguzi.
Lema aliandika ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa Jafo anatakiwa kuchunga kinywa chake kuhusu mambo muhimu yanayohusu ustaarabu , mshikamano, utawala bora na ustawi wa nchi.
Alisema duniani kote dhuluma katika uchaguzi zimekuwa ni sababu za uvunjifu wa amani. “Kuna siku mtalipa gharama za matendo yenu,” alisema Lema.
Lema aliandika ujumbe huu”Waziri Jafo acha kuongea kama kijana anaye balehe, chunga kinywa chako kuhusu mambo muhimu yanayohusu ustaarabu, mshikamano, utawala bora na ustawi wa nchi , Duniani kote dhuluma katika uchaguzi zimekuwa sababu za uvunjifu wa amani. Kuna siku mtalipa gharama za matendo yenu,” alieleza Lema.
Chadema jana ilitangaza uaamuzi wake wa kutokushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kutokana na figisu mbalimbali walizofanyiwa, hivyo hawapo tayari kuendelea na mchakato huo.
baada ya kutolewa kwa taarifa hiyo, Jana Waziri Jafo alisema ameshangazwa na kitendo cha Chadema kujitoa katika uchaguzi wakati kanuni zinawapa zipo wazi zinamruhusu mtu yoyote kukata rufaa
Waziri Jaffo,acha kuongea kama kijana anaye balehe,chunga kinywa chako kuhusu mambo muhimu yanayohusu ustarabu,mshikamano,utawala bora na ustawi wa Nchi,Duniani kote dhuluma ktk chaguzi zimekuwa sababu za uvunjifu wa amani.Kuna siku mtalipa gharama za matendo yenu— Godbless E.J. Lema (@godbless_lema) November 7, 2019