Maalim Seif aeleza anachojutia kwa Lipumba


Mshauri Mkuu wa Chama Cha ACT - Wazalendo, Maalm Seif Sharif Hamad, amesema moja ya mambo anayoyajutia ni kumuamini Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba, wakati akiwa Katibu Mkuu wa chama hicho.


Maalim Seif ametoa kauli hiyo, wakati akizungumza kwenye kipindi cha KONANI cha kituo cha Televisheni cha ITV kupitia kurasa zake za Facebook na YouTube, ambapo amesema sababu ya kumuamini Lipumba ndiyo imepelekea CUF kumeguka.

Maalim Seif amesema kuwa "jambo nililolifanya ninajutia ni kumuamini Lipumba nilipata maneno kutoka wa Wazee kuhusu Lipumba lakini mimi niliendelea kumuamini, ndiye aliyetukifikisha hapa kukigawa chama mpaka sisi tukachukua maamuzi ya kuondoka."

Maalim Seif aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), lakini alifikia maamuzi ya kukihama chama hicho baada ya kuibuka kwa mgogoro baina ya CUF iliyokuwa ikimuunga mkono yeye, na upande uliokuwa ukimuunga mkono Prof Lipumba.

Baada ya mgogoro huo kudumu kwa muda mrefu ilifunguliwa kesi Mahakama Kuu ya Tanzania, ili Mahakama, ieleze kuhusu kutambuliwa kwa Lipumba, ambapo March 18, 2019 Mahakama ilisema Lipumba ni Mwenyekiti halali wa chama hicho.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad