Maambukizi ya virusi vya UKIMWI tishio Morogoro
0
November 14, 2019
Hali ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi katika Manispaa ya Morogoro yamefikia asilimia 4.5, Hii ni kwa mujibu wa taarifa zilizokusanywa kwenye vituo vya afya na huduma ya mkoba.
Taarifa hizo zilitolewa juzi na mratibu wa Ukimwi wa Manispaa hiyo, Pendo Elias kwenye kikao cha maandalizi ya Siku ya Ukimwi Duniani, amesema mwaka huu mbali ya kutoa huduma ya kupima virusi vya Ukimwi, kutakuwa na huduma ya upimaji saratani ya shindo ya kizazi, kisukari na shinikizo la damu.
Bi. Pendo amesema elimu itatolewa kwa makundi tofauti ya watu wakiwamo vijana ambao ndiyo kundi kubwa linaloonekana kuathirika.
Naye, Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Morogoro, Michael Waluse alisema takwimu za maambukizi ya Ukimwi za manispaa hazipendezi hivyo lazima kila mdau aweke nguvu ya kupambana na maambukizi mapya badala ya kuachia kazi hiyo Halmashauri.
Tags