Maandamano ya Iran: Video zafichua ukatili ambao utawala ulijaribu kuificha dunia


Video moja iliyochukuliwa kupitia mlango wa nyumba inaonekana ikimuonesha mwanamke akimtazama kijana mmoja mdogo akiwa amelala kwenye damu kando ya barabara, huku watu waliokuwa wakiwakimbia polisi wakipita na kumkanyaga chini.

Nyingine iliyochukuliwa kutoka katika mji wa kusini wa Shiraz ulionesha umati wa watu wakijaribu kumsaidia mtu ambaye amepoteza fahamu aliyekuwa amelala chini huku watu wengine wakijaribu kuutoroka mtaa uliokuwa umejaa moshi na sauti zikisikika za watu waliokuwa wakipiga kelele kwa hofu pamoja na milio ya risasi.

Mawasiliano ya mtandao yarudishwa Iran
Hofu ya vifo yatanda katika maandamano Iran
Kwa nini maandamano ya Iran ni tofauti?
Ya tatu , ilichukuliwa kutoka ndani ya gari lililokuwa likiendeshwa katika mji mkuu Tehran, ambamo mwanamke aliweza kusikika akipiga mayowe huku mapolisi waliokuwa wamevalia sare wakimtia nguvuni mwanamume

Ilikuwa ni hofu ya picha za aina hiyo ambazo ziliwafikia wakazi wa maeneo ya dunia ambazo ziliwachochea maafisa wa Iran kufunga intaneti kwa zaidi ya siku nane mapema mwezi huu , wakati maandamano dhidi ya ongezeko kubwa ka bei ya mafuta yaliposambaa kote nchini humo. Na sasa intaneti imerejeshwa kwa muda , video zimekuwa zikionekana kwenye miytandao ya kijamii zinazoonyesha ukatili wa serikali katika kuzima maandamano kuwa mkubwa kuliko ilivyohofiwa awali . Utambulisho na hadithi za waandamanaji waliopoteza maisha yao zimejitokeza.

Maafisa wa Iran hawajatoa idadi yoyote rasmi ju ya watu waliokufa na majeruhi , lakini shirika la haki za binadamu la Amnesty International limepokea kile linachokiamini kuwa ni taarifa za kuaminika kwamba waandamanaji takriban 143 waliuawa baada ya kulipuka kwa maandamano tarehe 15 Novemba.

Shirika hilo la haki za binadamu linasema vifo husababishwa zaidi na matumizi zaidi ya silaha ya vikosi vya usalama dhidi ya waandamanaji - ingawa limeripoti kuwa mtu mmoja alikufa baada ya kuvuta hewa ya gesi ya kutoa machozi na mwingine baada ya kupigwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad