Maeneo ambayo upinzani umeshinda Uchaguzi serikali za mitaa yawekwa wazi
0
November 28, 2019
Waziri wa nchi, ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na Serikali za mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo ameanisha baadhi ya maeneo ambayo vyama vya upinzani vimeshinda kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa licha ya viongozi wao wakuu kutangaza kujiondoa kwenye uchaguzi.
Jafo ametaja mikoa na wilaya ambazo wapinzani wameshinda kuwa ni Kagera (Muleba DC), (Kibondo), Mara (Rorya), Rukwa (Sumbawanga DC), Nkasi DC na Sumbawanga manispaa, Tabora (Igunga na Kaliua DC).
Chadema kimeshinda vitongoji 27 katika mikoa mitano ikifuatiwa na CUF na ACT – Wazalendo kilichopata kitongoji kimoja katika mikoa hiyo.
Kwa upande wa vijiji amesema vyama vya upinzani vimeshinda nafasi katika mikoa mitatu ya Kigoma, Kagera, Rukwa katika halmashauri ya Kibondo, Muleba na Nkasi.
Chadema wamepata kijiji cha kitoko (Muleba) kilichopo kata ya Mubunda na vijiji vya kasu na Ntamila vilivyoko wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa.
chama kingine kilichoshinda ni CUF katika kijiji cha Kumkungwa kilichopo wilayani Kibondo.
Mkutano wa 39 wa Baraza la Mawaziri wa EAC kuanza kesho jijini Arusha
Na vitongoji, Chadema imeshinda kagera (9), vyote wilaya ya Muleba, Kigoma (3) katika wilaya ya Kibondo, Mara (2), Rukwa (8) na Tabora (5).
Vyama vingine ni CUF walioshinda Kagera (1), Kigoma (1), na Tabora (1), ACT wazalendo wamepata kiti kimoja tu mkoani Kigoma.
Tags