Rais Magufuli "Vya Bure Vimeisha...Sikuja Kuleta HELA Mfukoni Kwako"


Rais John magufuli amewaambia wananchi wa Wilaya Igunga kuwa hakuja kuleta fedha mifukoni mwao na vya bure vimeisha na kuwataka kufanya kazi na sio kulalamika.

“Vya bure vimeisha na bado vitaisha zaidi, ndugu zangu vya bure hakuna hata mimi sina vya bure, wewe unataka mkono wako uwe soft haufanyi kazi alafu unataka hela, mimi sikuja kuleta hela mfukoni mwako, nimekuja kuwaambia ukweli fanyeni kazi, sio kulalamika tu”alisema Rais.

Rais alieleza hayo baada ya mwananchi Abel Mbinga kumuomba Rais Magufuli kuachia fedha mengine yote hawana shida naye kwani hilo likikamilika hata akitawala milele hakuna shida.

“Rais kama itakupendeza maisha ni magumu sana, fedha hakuna watu wana hali mbaya, akina mama wananyang’anywa TV kwa ajili ya mikopo tunaomba uachie fedha, mengine yote hatuna tatizo na wewe yakikamilika hayo hata ukitawala milele haina shida,” alisema Mbinga

Tags: #RaisMagufuli, Asemahakunavyabure, Fanyakazi
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad