Mahakama Kutoa Uamuzi dhidi ya Mshtakiwa Kusafiri nje Dar


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam nchini Tanzania imepanga Novemba 18, 2019 kutoa uamuzi iwapo mshtakiwa Charles Newe, ataruhusiwa kusafiri nje ya mkoa wa Dar Es Salaam au laa.

Newe na wenzake wanne, akiwemo Mkurugenzi wa Kampuni ya Huduma za Usafirishaji wa Mabasi yaendayo Haraka, maarufu Mwendokasi (Udart), Robert Kisena, wakabiliwa na mashtaka 15, yakiwemo ya kuisababishia UDART hasara ya Sh 2bilioni.

Hatua hiyo inatokana na mshtakiwa huyo kuwasilisha ombi mahakamani hapo akiomba kupewa kibali cha kusafiri nje ya mkoa wa Dar es Salaam.

Newe aliwasilisha ombi hilo mbele ya Hakimu Mkazi, Vicky Mwaikambo, wakati kesi hiyo ilipoitwa mahakamani hapo.

Kupitia wakili wake, Nehemia Nkoko, mshtakiwa huyo alidai kuwa anaiomba mahakama hiyo impatie kibali cha kusafiri kwenda mkoani Njombe na Morogoro kwa ajili ya shughuli zake za kibiashara.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad