Mahakama Yaamuru Heche, Msigwa, Bulaya, Mdee Wakamatwe


KUFUATIA Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wiki iliyopita kuamuru wabunge wanne wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakamatwe na kufikishwa mahakamani hapo kwa kukiuka masharti ya dhamana, wabunge hapo wametolewa mahakamani hapo leo Jumatatu, Novemba 18, 2019 na kupelekwa katika Kituo cha Polisi, Oysterbay jijini Dar es Salaam.



Wabunge hao ambao ni washtakiwa katika kesi ya uchochezi namba 112 ya mwaka 2018 ni; Ester Bulaya (Mbunge wa Bunda Mjini), John Heche (Mbunge wa Tarime Vijijini), Peter Msigwa (Mbunge wa Iringa Mjini) na Halima Mdee (Mbunge wa Kawe).



Amri ya kukamatwa ilitolewa Novemba 15, 2019, na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kufuatia washtakiwa hao kutofika Mahakamani hapo wakati kesi yao ilipokuja kwa ajili ya kusikilizwa ushahidi upande wa utetezi bila ya kuwepo taarifa zozote kutoka kwao wala wadhamini wao.



Juzi, Novemba 16, Halima Mdee, alijisalimisha katika Kituo cha Polisi Oyster Bay, kufuatia agizo hilo la mahakama. Wabunge hao pamoja na wenzao watano akiwemo mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, wanaotuhumiwa kwa kufanya maandamano yaliyosababisha kifo cha Mwanafunzi wa NIT, Akwilina Akwilin.



Amri hiyo ya kukamatwa kwa wabunge hao Halima Mdee, Peter Msigwa, John Heche na Ester Bulaya, ilitolewa jana, Novemba 15, 2019 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba, ambapo alisema kuwa kesi hiyo ilifikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya upande wa mashtaka kumhoji Mbowe na baada ya kumaliza kutoa ushahidi wake kutoka upande wa utetezi na ndipo ilipobainika washtakiwa hao wanne kutowepo mahakamani.



Baada ya kutoa agizo hilo hakimu ameiahirisha kesi hiyo hadi Novemba 21, 22 itakapoendelea na upande wa utetezi kuendelea na ushahidi wao.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwa hivyo, Amri ya Mahakama imeteekelezwa na hawa watatuwamesha wekwaRumane kama alivyo Mdee?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Inaelekea, vijana wa Sirro wanasusua,labda litatoka tamko leo juu ya Utekelezaji.

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad