Mahakama Yaamuru Tundu Lissu Afike Mahakamani Disemba 19


Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Thomas Simba ameagiza aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, afike Mahakamani kesi yake itakapotajwa tena mnamo Disemba 19 Mwaka huu baada ya
Mdhamini wake kutoa uthibitisho wa Maendeleo ya Lissu Mahakamani

Alipokuwa akitoa uthibitisho huo Mdhamini wa Lissu, Ibrahim Mohamed aliieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa Lissu  amepona lakini amesema hawezi kurudi Nchini kwa sababu ya kuhofia usalama wake.

Hakimu Simba alimkatisha na kumueleza kuwa; "Sisi hatutaki siasa hapa, namtaka Mshtakiwa, naahirisha kesi hadi December 19,mwaka huu siku hiyo nataka Lissu awepo."

Mbali na Lissu washtakiwa wengine ni, wahariri Simon Mkina, Jabir Idrisa na mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehbooh.

Kwa pamoja washtakiwa hao, wanakabiliwa na mashtaka matano ikiwamo kuandika habari za uchochezi kinyume na Sheria ya Magazeti ya mwaka 2002.

Ilidaiwa kuwa kati ya Januari 12 hadi 14, 2016 jijini Dar es Salaam, washtakiwa Jabir, Mkina na Lissu, waliandika na kuchapisha taarifa za uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho, 'Machafuko yaja Zanzibar.'

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad