Makonda afichua siri ya Magufuli kwa miaka 50
0
November 18, 2019
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, amesema Rais John Pombe Magufuli amevunja rekodi kwenye ujenzi wa mtandao barabara wa Lami nchini tangu Tanzania ilipopata uhuru, kwa kujenga mtandao wa Lami wenye urefu wa Kilometa 807, huku katika kipindi cha miaka 50 zikiwa zimejengwa
Kilometa 402 tu.
Paul Makonda ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na viongozi wa Dini, jijini Dar es salaam, akiwaelezea kuhusiana na utendaji kazi wa Rais Magufuli kwa miaka 4, ambapo amesema moja ya sababu iliyopelekea kufanya hivyo ni Rais Magufuli kumtanguliza Mungu.
"Rais Magufuli tangu ameingia madarakani kajenga mtandao mpya wa Lami nakuvunja rekodi ya miaka yote 50 ya uhuru, amejenga Kilometa 807 mpya ndani ya miaka 4, ukilinganisha kwa miaka yote 50 tulijengewa Kilometa 402." amesema Makonda.
"Kawafanya viongozi wa Serikali wanaoingia na waliopo wanaotumia hirizi na wao wanamtaja Mungu kwanza, kwa lugha nyingine Rais Magufuli ni miongoni mwa watumishi wa Mungu katika nchi yetu ya Tanzania" ameongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda.
Katika Mkutano huo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, aliwaonesha kazi mbalimbali zilizofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli.
Tags