Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda jana Novemba 1, 2019 amefanya ukaguzi wa barabara ya Makongo Juu ambayo imekuwa ikilalamikiwa na wananchi wa eneo hilo kwa muda mrefu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wabarabara hiyo makonda amedai kuwa changamoto kubwa ni uongozi wa eneo hilo ukianzia na Mbunge ambaye hana huwezo wa kujenga hoja Bungeni, akiingia anakoroma na matusi juu.
Paul Makonda amezindua ujenzi wa barabara iliyokuwa kero kwa muda mrefu yenye urefu wa Km 4.5 kutoka Makongo Juu hadi Goba, ujenzi utakaogharimu kiasi cha Shilingi bilioni 8.9.
“Mmekula vumbi, mmeharibikiwa magari yenu pia mmechelewa makazini nawapeni pole sana wakazi wa Makongo, mkiwa na Viongozi ambao wanaheshimu Viongozi wengine mahusiano hayo yanapelekea mpate Maendeleo, lakini mkiwa na Viongozi wanaotukana Viongozi wengine mnabaki kuendelea kula vumbi, tunataka Makongo tuwawekee mpaka na taa, tunataka tujenge Barabara ya kisasa Makongo vumbi iwe historia na muonje pia na taa za Barabarani kama Masaki na sehemu nyingine”