Waliobaka Waachiwa HURU Kwa Kuwa Hawakutumia Nguvu Kubaka



Mahakama moja Nchini Uhispania, imewaachia huru Wanaume watano ambao awali walihukumiwa kifungo kwa kumbaka kwa zamu msichana wa miaka 14

Mahakama imeamua kwamba, hawakutekeleza ubakaji kwa kuwa mwathiriwa alikuwa katika hali ya kupoteza fahamu na kwamba hawakulazimika kutumia nguvu

Chini ya sheria za Uhispania, shtaka linaweza kuwa la ubakaji iwapo nguvu ama vitisho vilitumika, lakini pia kuna harakati ya kuirekebisha sheria hiyo

Makundi ya Haki za Binadamu yamepinga vikali uamuzi huo ambapo awali Washtakiwa walipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha kati ya miaka 15 hadi 20

Katika Utetezi wake wa awali msichana huyo aliyekuwa ametumia kilevi wakati wa tukio alisema alikumbuka kidogo yaliofanyika na mmoja wa Wanaume hao alikuwa akishikilia bunduki

Washukiwa wote walikana madai hayo, licha ya kwamba vinasaba vya mmoja wa Wanaume hao vilipatikana katika nguo ya ndani ya msichana huyo
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad