Marekani, Korea Kusini kusitisha Mazoezi Ya Kijeshi
0
November 18, 2019
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Mark Esper amesema kwamba wamesitisha kwa muda usiojulikana mazoezi ya pamoja ya kijeshi na Korea Kusini katika kile alichokitaja nia njema kuelekea Korea Kaskazini.
Hatua hiyo inakuja hata baada ya Waziri wa Ulinzi wa Japan Taro Kono ambaye nchi yake imekuwa ikitishwa na majaribio ya mara kwa mara ya makombora yanayofanywa na Korea Kaskazini kumuelezea Esper kwamba hakuna ambaye ana matumaini kuhusu kubadilisha hatua za Korea Kaskazini.
Matamshi hayo ya Kono yanaashiria kuzorota kwa mahusiano kati ya Marekani na washirika wake wa kimataifa, katika wakati wanapojaribu kuirejesha Korea Kaskazini kwenye mazungumzo ya kuachana na mipango yake nyuklia na makombora.
Ingawa katika tawala zilizopita Marekani iliyaita mazoezi hayo kuwa ni muhimu lakini Rais Donald Trump ameyaita kuwa ni upotevu wa fedha na uchokozi dhidi ya Korea Kaskazini.
Tags