Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amekemea tabia ya Wananchi wa wilayani Kilosa kuuza mashamba yao waliyopewa na Rais John Pombe Magufuli mara baada ya kubatilishwa kutoka katika mashamba pori.
Waziri Lukuvi amekemea tabia hiyo alipokuwa wilayani Kilosa mkoani Morogoro katika ziara yake ya utatuzi wa migogoro ya ardhi.
Amesema baadhi ya wananchi wamekuwa wakiuza maeneo yao kwa tamaa ya pesa na mali halafu baadae wanaleta migogoro ya ardhi kwa kutaka mashamba mengine.
Wakati huo huo Wananchi wa kijiji cha Magomeni kilichopo tarafa ya Kilosa Mjini wilayani Kilosa mkoa wa Morogoro wametoa kilio chao kwa Waziri Lukuvi wakitaka kupatiwa shamba la Mwekezaji Farm Africa Agro Focus Ltd marufu kama kwa Karamagi kwa madai kuwa mwekezaji wa shamba hilo ameshindwa kuliendeleza.
Wananchi hao wamemueleza Lukuvi kuwa kijiji hicho hakina ardhi ya kutosha kuwawezesha wananch hao kujishughulisha na kilimo na eneo kubwa katika kijiji hicho ni eneo la shamba la Farm lenye ukubwa wa ekari 13,000 ambapo Waziri Lukuvi alitatua hilo.
Marufuku Kuuza Ardhi Iliyotolewa na Rais Magufuli - Waziri Lukuvi
0
November 11, 2019
Tags