Miaka 23 imepita tangu kifo cha Tupac Shakur ambaye alipigwa risasi September 7, 1996 lakini mpaka leo hakuna mtu yeyote aliyekamatwa.
Akizungumza na idara ya polisi mjini Los Angeles jamaa aitwaye Duane "Keffe D" Davis member wa kundi la Crips aliwahi kukiri kuhusika na mauaji ya Tupac Shakur. Lakini kutokana na masuala kadhaa ya kisheria ambayo yalizunguka kesi hiyo, hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.
Sasa Greg Kading, askari wa zamani wa LAPD ambaye pia alikuwa sehemu ya jopo la uchunguzi wa mauaji hayo na ndiye aliyefanya mahojiano Keffe, amezungumza na BET Death Row Chronicles na kusema sheria ifatwe na Keffe akamatwe.
Moja ya ushuhuda wa Keffe ni alithibitisha kwamba mpwa wake aitwaye Anderson ndiye aliyempiga risasi Tupac, na silaha alimpatia yeye [Keffe D] wakiwa pamoja kwenye gari. Anderson kwa sasa ni marehemu, aliuawa Mei 1998.