Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe ameshindwa kujitetea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akiomba apumzike kutokana na matatizo ya Kiafya ikiwemo kusumbuliwa na ugonjwa wa Dengue, Malaria na Shinikizo la Damu.
Mbowe na Viongozi wenzake nane wa CHADEMA wanakabiliwa na mashtaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia na kuhamasisha hisia za chuki.
Wiki iliyopita Mbowe aliripotiwa kuugua na kulazwa katika Hospitali ya Aga Khan na leo November 26,2019 amefika Mahakamani hapo lakini kupitia Wakili wake Peter Kibatala ameeleza kuwa hali yake kiafya bado si nzuri na anahitaji kupumzika.
Hakimu Simba amesema kuwa afya ya Mshitakiwa ni jambo la msingi hivyo ameahirisha kesi hiyo kwa siku mbili ambapo itaendelea November 28, 29 na Desemba 2, 3 na 4, mwaka huu kwa ajili ya kusikilizwa.