Mbunge wa Ndanda ataka kumrithi Mbowe


Mbunge wa Ndanda kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Cecil Mwambe, ametangaza rasmi ridhaa yake ya kugombea nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho kwa lengo la kumpokea kijiti, Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Freeman Mbowe.



Mwambe ameyabainisha hayo leo Novemba 26, 2019, Jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza mbele ya Wandishi wa Habari, ambapo amesema kuwa licha ya kukutana na maneno ya kejeli na masimango lakini nia yake bado ni ileile na kamwe hatoweza kujitoa kugombea nafasi hiyo.

"Nilianza kuona nina haja ya kugombea baada ya kumshuhudia Mwenyekiti wa chama chetu Mh Mbowe akituambia kwamba, asingependa aendelee kuwa Mwenyekiti wetu na kwamba anatamani angeacha nafasi hiyo kwa mtu mwingine ili aendeleze yale mazuri aliyafanya, nikaona ipo haja ya kumpokea kijiti hasa baada ya kueleza kwa kina madhira ambayo amepitia kwa vipindi vilivyotangulia nikaingiwa na huruma" amesema Mwambe.

Uchaguzi wa ndani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),unatarajiwa kufanyika Desemba 18, 2019.


Ukweli kuhusiana na rasta alizo nazo Mrisho Mpoto | East Africa
|

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad