Mfahamu Mwanamke anayeishi na Sehemu mbili za Uke



Elizabeth Amoaa ni mwanamke ambaye amezaliwa akiwa na sehemu mbili mbili za uzazi ikiwa ni pamoja na kuwa na sehemu mbili za uke, njia mbili za uzazi na mifuko miwili ya Uzazi

Mwanamke huyu mzaliwa wa Ghana ambaye kwasasa anaishi Walsall, Birmingham Uingereza aligunduliwa akiwa na hali hiyo miaka mitano baada ya kujifungua mtoto wake Rashley ikiwa ni zaidi ya miaka 21 ya kwenda na kurudi hospitali bila kugundulika tatizo lake.



Elizabeth Amoaa na bintiye Rashley
Elizabeth amekuwa akisumbuliwa sana na Tumbo hususan akiwa katika siku zake za mwezi hali iliyokuwa ikimpelekea mpaka kupoteza fahamu huku kwa muda mrefu na katika hospitali tofauti tofauti akiambiwa kuwa ana tatizo la mayoma hivyo hatoweza hata kupata mtoto.

Mwaka 2010 alipopata ujauzito ilikua ni taarifa ya kushangaza kwa kila mtu aliyemfahamu kutokana tayari taarifa za kidaktari zilionesha uwezekano wa kupata mtoto haupo.

Safari ya miezi tisa haikuwa rahisi kwake kwani katika kipindi cha ujauzito alikabiliwa na utokaji wa damu sana, kupoteza fahamu na uchovu usiomithilika. “Ulikuwa ni ujauzito wa changamoto kubwa, nilikuwa natokwa na damu muda wote, uchovu mwingi na wakati mwengine nilikua napoteza fahamu” anaeleza Elizabeth

“Madaktari walidhani ujauzito umetunga nje ya fuko la uzazi kwasababu sote hatukujua kama nina mafuko mawili”. Anafafanua Elizabeth. “Pia nilipokuwa nikifanyiwa skanning kutizama maendeleo ya mtoto tumboni wakati mwengine walimuona na wakati mwengine hawakukuta kitu kwasababu walitizama kwenye fuko tofauti na alilokwepo mtoto na hawakuweza kudhani kuwa nina mafuko mawili kutokana kwamba si kawaida kutokea tatizo hili”

Kutokana na tatizo la kutokuonekana mtoto madaktari walishauri waukatishe ujauzito huo lakini Elizabeth alikataa kwakuwa alikua anahisi kuna mtoto na hali ya tumbo lake kukuwa alimfanya avute subra kuona litakalotokezea.


Mume wa Elizabeth na Binti yao
Akiwa ametimiza wiki ya 32 katika ujauzito wake, Elizabeth alijifungua mtoto wa kike huku madaktari na watu wanaomzunguka wakipigwa na butwaa na kuona ni muujiza wa hali ya juu.

Mwaka 2015 kipimo cha MRI kilionesha kwamba Elizabeth ana mafuko mawili ya uzazi. “Ilinishangaza kwani sikuwahi kusikia kuwa kuna mtu ana mafuko mawili ya uzazi na mwaka 2016 walinifanyia upasuaji na kugundua pia ni njia mbili za uzazi na sehemu mbili za uke”

Kwasasa Elizabeth ameanzisha Taasisi inayojishughulisha na utoaji wa elimu kwa watoto wa kike kuhusiana na afya ya uzazi kwa wanawake.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad