Mwanamitindo Miriam Odemba ambaye kwa sasa ametimiza miaka 22 kwenye tasnia ya mitindo, akiwa amefanikiwa kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika anga la kimataifa, mrembo huyo mwenye makazi yake nchini Ufaransa hivi sasa amerejea nchini kufanya shughuli za kijamii kupitia taasisi yake ya Miriam Odemba Faundation.
Hivi karibuni mrembo huyo alitembelea shule ya kiwambo mkuranga pwani kuzindua kisima cha maji katika shule hiyo.
Aidha amesema katika miaka 22 ya kuwepo kwenye tasnia ya mitindo amefanikiwa na anamshukuru Mungu pia ameokoka na kwasasa anafanya kazi ambayo inayaweza kuwasaidia wadogo zeke waweze kufuata nyayo zake.
Ameongeza kuwa yeye hajapata elimu kubwa ya darasni lakini “nimepata elimu ya maisha nimefunzwa na ulimwengu na nimetembelea nchini nyingi sana na ndiyo maana sasaivi nasaidia kina mama na watoto kwa sababu wao ndiyo nyumba ya taifa”.
”Nimeanza mitindo nikiwa na umri wa miaka 16 nikaenda nchi za nje huko ndiyo mafaniko yangu nikaanza kuyaona, nimetoka familia ya kimasikini na nilipata uchungu nikasema malengo yangu lazima niyatimze nikipata tu pesa” alisema Odemba.
Hata hivyo mrembo huyo amewashauri warembo wa tanzania kutazama vitu anavyofanya na kama wanataka kushirikiana na yeye milango ipo wazi atawapa siri kubwa ya kuisaidia jamii maana peke yake hataweza.