Mume wa Zamaradi Aitwa Kuripoti Polisi Baada ya Kumtishia Kumpiga Mtu Bastola



Inspekta Jenerali wa Polisi nchini Tanzania (IGP), Simon Sirro amemtaka kijana aliyemtishia mwenzake bastola kuripoti polisi baada ya kuonekana akifanya kitendo hicho katika picha za video zinazosambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii nchini.

Mbali na kuripoti, Sirro amesema anatakiwa kusalimisha silaha yake.

Ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya hafla ya uzinduzi wa kampeni ya Utatu inayolenga kukomesha rushwa barabarani.

Sirro amesema ameagiza kukamatwa kwa kijana huyo lakini amekuwa akipiga chenga,  amemtaka akajisalimishe mwenyewe kituo cha polisi na kufikishwa mahakamani.
IGP Sirro azungumza na waandishi wa habari baada ya uzinduzi rasmi wa kampeni ya kukomesha rushwa barabarani

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad